bokomslag Mwana-Adam ni Nani Naye ni Nini Mungu Amkomboe
Filosofi & religion

Mwana-Adam ni Nani Naye ni Nini Mungu Amkomboe

Shannel S Silwimba

Pocket

399:-

Funktionen begränsas av dina webbläsarinställningar (t.ex. privat läge).

Uppskattad leveranstid 5-10 arbetsdagar

Fri frakt för medlemmar vid köp för minst 249:-

  • 188 sidor
  • 2023
Kitabu hiki MNNNMA ni kiberiti kinacho washa moto wa mabadaliko makubwa, na kama siyo mapinduzi ndani ya kanisa lote linalo zungumza Kiswahili. Katika hiki tunaona mtizamo mpya wa theolojia, changamoto katika tafsiri za biblia ndani ya lugha ya Kiswahili, na jipya zaidi ni uhamisho wa waumini toka udini kuelekea mahusiano na Mungu YHWH.Kitabu kinachukulia biblia yote kuwa fumbo la picha, na hivyo kutumia mstari wa wakati uendao mbele katika mduara, kuonyesha mwanzo hadi mwisho wa kila kitu. Na kama hili halitoshi, kinaweka dai tatanishi kwamba, biblia yote iliandikwa kwa ajili ya ukombozi wa Adonai Yeshua Kristo, na kwamba yote humo pamoja na maisha yako yote, ni kwa ajili ya Mungu YHWH kuwa na familia yake tu.Kitabu kinacho dai tete la kuifunua kweli iliyo moja na ya pekee mahali pote, wakati wote, na kwa vizazi vyote. Na katika kunogesha uelewa; kinapinga mafundisho yaliyo zoeleka kwamba, mtu ataishi Mbinguni na Mungu milele, kwa kudai maandiko yote yanasema, ni Mungu YHWH anaye hamia katika Dunia mpya ndani ya Yerushalem Mpya kuishi humo milele na watoto wake watakatifu.Kitabu kinajikita katika malumbano ya kidini na sayansi, na kuitumia teknolojia ya sasa kuelezea dhana nyingi za kiimani. Na kwa kila funzo la kinadharia unalo pewa, pia huonyeshwa jinsi ya kutenda hilo uhesabiwe mstahiki wa ahadi hiyo ya Mungu. Na katika ujasiri mkuu kinaweka dai ya kuwa, hicho ni ujumbe halisi wa Mungu YHWH kwa kanisa lake tukufu linalo zungumza Kiswahili.Ni kitabu ambacho kila anayefunza dini hawezi kukikosa, na kwa kila mtu anaye taka kujua kweli ya mambo ya kiungu, hiki ni kitabu muhimu zaidi sokoni kwa sasa. Tunakiona kutawala malumbano katika kumbi za mihadhara, mimbari za masinagogi, na hata madarasani kufunzwapo dini. Ni kitabu ambacho kitafungua jicho la kila muumini, kwani katika lugha ya Kiswahili hakipo kinacho zama katika kina chake hiki. Kwa kweli uhamsho wa kanisa linalo zungumza Kiswahili sasa umefika wakati wake!

  • Författare: Shannel S Silwimba
  • Format: Pocket/Paperback
  • ISBN: 9798215259061
  • Språk: Swahili
  • Antal sidor: 188
  • Utgivningsdatum: 2023-01-25
  • Förlag: Shannel S Silwimba