bokomslag Nimebadilika 2011
Skönlitteratur

Nimebadilika 2011

Dardanus Mfalme

Pocket

279:-

Funktionen begränsas av dina webbläsarinställningar (t.ex. privat läge).

Uppskattad leveranstid 7-12 arbetsdagar

Fri frakt för medlemmar vid köp för minst 249:-

  • 140 sidor
  • 2011

Ni kitabu chenye hazina ya tungo zilizotungwa na mtunzi mahiri aliyebobea katika fani ya utunzi wa mashairi, tenzi, ngonjera na nyimbo. Mtunzi wa kitabu hiki amejumuisha tungo alizozitunga hivi karibuni na zile alizozitunga kitambo nyuma hivyo kikifanya kitabu hiki kiwe na hisia tofauti tofauti.


Tofauti na vitabu vingine ama watunzi wengine, upekee wa kitabu hiki ni kwamba, mtunzi wake ameonyesha umahiri wa kucheza na lugha kwa kuchanganya maneno ya Kiswahili sanifu, Kiswahili cha mitaani na maneno aliyoyatohoa katika lugha nyingine mbalimbali ambayo hutumiwa kwa wingi katika jamii ya sasa, na ndio sababu hasa amekiita kitabu hiki "Mashairi ya Kisasa"


Burudani kamili inapatikana ndani ya kitabu hiki katika sehemu ya malumbano ambapo mtunzi wa kitabu hiki amejibizana na washairi wengine waliobobea wakiwemo Shehe Hadji Saeedia, Stephen S. Mkoloma, Sharifa Bakari, Linda Ndalu, Ndugu Chilewa, Omari Njenje na Ndugu Mgimba.


Kama ilivyo ada yake, katika kurasa za mwisho wa kitabu hiki mwandishi ameweka kamusi ya Kiswahili cha mitaani ili kila asomaye kitabu hiki apate burudani kamili asomapo ama aimbapo tungo zake.

  • Författare: Dardanus Mfalme
  • Format: Pocket/Paperback
  • ISBN: 9781462051090
  • Språk: Swahili
  • Antal sidor: 140
  • Utgivningsdatum: 2011-10-21
  • Förlag: iUniverse